CHAMA CHA WALIMU TANZANIA (CWT) KIMEOMBA KUKUTANA NA SERIKALI KABLA SHULE HAZIJAFUNGULIWA.
Posted on
Aug 17, 2012
|
No Comments
Gratian Mukoba Rais wa Chama cha walimu CWT
Chama cha walimu Tanzania (CWT) kimeomba serikali kufanya mazangumzo na cha hicho yenye lengo la kujadili madai ya waalimu kabla ya shule za misingi na sekondari hazijafunguliwa mapema mwezi ujao.
Kauli hiyo imetolewa juzi na kaimu katibu Mkuu wa CWT Taifa Ezekiel Olioch wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Sumbawanaga.
Alieleza kuwa chama cha walimu kitaendelea na mgomo kupitia waalimu mpaka hapo serikali itakapofanya mazungumzo na chama hicho na kulipwa asilimia zenye tija.
“Hata kama walimu watafika kwenye shule zao baada ya kufungua mwezi ujao kama mazungumzo na serikali yatakuwa bado hayajafanyika mgomo huo utaendelea na walimu hawatakuwa na ari kufundisha” alisema Olioch.
Alieleza njia pekee ya kumaliza tatizo la walimu ni serikali kukaa na chama cha walimu na kujadiliana madai yao.
Aidha chama hicho endapo watasikilizwa madai yao wao wako tayari kulipwa asilimia ambazo wanaona zina wafaa si lazima ziwe kama walivyoomba awali.
Alisema walimu hawakubaliani na kiwango kilichoongezwa cha mshahara wa waalimu kwa asilimia 12.12 ambazo ni sawa na shilingi 32,600/=
Pia alisema chama cha walimu Tanzania (CWT) kimesikitishwa na kauli zinazotolewa na baadhi ya viongozi wa siasa kuwa chama hicho cha walimu kinafadhiliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
“Tunapenda kuwahakikishia CWT haina ufadhiri wowote wanaoupata kupitia kwa chama hicho cha siasa hivyo wanaomba mawazo hayo potofu ni ya uchonganishi” alisema
Kwa upande wa Mkoa wa Rukwa na Katavi wenye shule za sekondarai 99 shule 96 zilishiriki katika mgomo na kwa upande wa shule za msingi 524 shule 491 walimu waligoma kabisa.