WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AWEKA JIWE LA MSINGI JENGO LA OFISI YA CAG MJINI DODOMA
Posted on
Aug 17, 2012
|
No Comments
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akiweka wa jiwe la msingi katika jengo la Ofisi ya Taifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali mjini Dodoma leo. Jengo hilo jipya lenye urefu wa ghorofa nane, linatarajiwa kuwa Makao Makuu ya Ofisi hiyo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, wakati alipowasili kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi katika Jengo hilo leo.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda , akipata maelezo kutoka kwa Meneja Ujenzi wa jengo hilo, Casmil Muscbi. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Rehema Nchimbi, watatu kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Athanas Pius .
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuweka wa jiwe la msingi katika jengo la Ofisi ya Taifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali mjini Dodoma litakalokuwa na urefu wa ghorofa nane na linatarajiwa kuwa Makao Makuu ya Ofisi hiyo.Picha zote na Magreth Kinabo- Maelezo