BARUA YANGU FUPI KWA MWALIMU NYERERE (R.I.P)
Posted on
Nov 11, 2012
|
No Comments
Dear
Mwalimu;
Tangu uondoke Tanzania hali imebadilika, siku hizi Mlima Kilimanjaro upo Kenya, Ziwa Nyasa lipo Malawi,Tanzanite ipo Kenya,Tanesco ni Rostam Aziz, Sheikh Ponda ndio IGP japo hajateuliwa na Rais na pia Rais wetu siku hizi anaishi Airport na historia imebadilika kuwa ule Muungano ulioasisi wewe na Karume ulitokana na Muungano wa Visiwa vya Pemba na Zimbabwe kuungana na Tanganyika mwaka 11964. Nasikia sikia eti na kaburi lako lipo Kenya. Wale maadui watatu wa taifa uliokuwa unapambana nao wewe yaani umaskini, ujinga na maradhi wote wamekuwa sugu mno ila serikali yetu inajaribu kupambana sana "adui" mmoja tu, Chadema.
Huyu wa sasa anatusumbua sana kwa sababu anataka kufanya nchi isitawalike kwa kuwashawishi Walimu na madaktari pamoja na wanafunzi wa Vyuo vikuu wadai haki zao. Juzi juzi tu huyu "adui yetu" alitaka kusababisha tupigane na jirani yetu Malawi kwa sababu ya uchochezi wake.
Leo hii kuna mkutano Mkuu huko Dodoma wa Chama ulichokiasisi wewe na ndugu yako Karume. Nasikia huko kuna moto na wajukuu zako eti wanamkataa Mwenyekiti wao. "Watu wenyewe wanaompinga Mwenyekiti "ni wahuni wachache kutoka Chadema". Hata hivyo kama kawaida hawatafua dafu, tutawadhibiti tu"- Ni nukuu toka kwa kiongozi mmoja wa Chama huko Dodoma.
Nilitaka kusahahu....kuna watu eti wanamiliki trilioni 16 nchini Uswisi na ni jana tu serikali ya mdogo wako JK kupitia kwa Lukuvi, Hawa Ghasia na Mwanasheria wa serikali wameomba majina kutoka kwa ndugu Zitto Kabwe ili serikali ichukue hatua wakati ndani ya serikali yao yupo Waziri Membe ambaye ana majina ya wenye akaunti hizo pamoja na wale wa "chenji" ya rada.
Kule Bungeni Baba, kuna maajabu yanaendelea. Eti Spika wa bunge ametoa onyo kali kwa niaba ya Bunge kwa mtu ambaye sio mbunge kwa kulisingizia Bunge. Kibaya zaidi aliyechunguza tuhuma za kuhongwa wabunge ni bunge lenyewe...Nisikuchoshe zaidi Mwalimu...pumzika kwa amani!!!