SABABU 5 CCM KUSHINDA UCHANGUZI 2015
Posted on
Nov 11, 2012
|
No Comments
Ndugu zangu ni
vizuri kuambiana mambo ya msingi haswa linapokuja swala la hatma ya Taifa letu.
Tanzania ni nchi ya kipekee duniani na watu wake ni wa kipekee pia, utu wetu , utanzania wetu huwezi pata sehemu nyingine. Watanzania ni watu wenye upendo, amani na mshikamano huwezi linganisha na nchi yoyote ile. Tumekuwa tukiishi siku zote kwa amani, kupendana na kushirikiana kabla na hata baada ya kuasisiwa taifa letu. Lakini baada ya kuingia siasa za upinzani nchini mwetu , kumekuwa na fikra zenye kuhatarisha amani yetu. Hatukatai upinzani, ndio maana kumekuwa na vyama vingi vya siasa nchini Tanzania. lakini kamwe hatutaruhusu amani yetu kupotea na siasa za kutubagua. Hadi hapa, Amani na maendeleo yaliyopoTanzania yametokana na uongozi wa chama cha mapinduzi. Kuanzia kwa wazee wetu waasisi, na viongozi wetu wakiongozwa na Mwenyekiti wetu, Rais wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete. Kwa siasa safi na uongozi makini, Sina budi kuzitaja sababu 5 kwa nini chama cha mapinduzi kitashinda uchaguzi wa 2015.
Moja; CCM imeweza kulinda na kudumisha Uhuru wa Nchi yetu na raia wake.
Muhimu kwa watanzania wote kukumbuka kwamba chama cha mapinduzi hakina udini wala ukabila kwa misingi hiyo kimeweza kudumisha amani na umoja wa nchi yetu.
Mbili; CCM imekuwa ya kwanza katika ushirikishwaji wa watanzania wote walio nje ya nchi katika kutoa mchango wao ili kuleta tija na maendeleo ya taifa letu.
Tatu; CCM imehakikisha kwamba Nchi yetu inatawaliwa kwa misingi ya kidemokrasia. Nchini Tanzania kuna demokrasia ya kutosha na hata kupitiliza. Mwananchi yoyote anao uhuru wa kuishi, kuabudu na kufanya maamuzi apendayo ili mradi sheria za nchi zinazingatiwa.
Nne; CCM haina ubaguzi, kila mtu anayo nafasi. Chama cha mapinduzi siku zote kimekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba Serikali na vyombo vyote vya umma vinatoa nafasi zilizo sawa kwa raia wote, wanawake na wanaume bila kujali rangi, kabila, Dini, au hali ya mtu.
Tano; CCM iko mstari wa mbele katika kuimarisha uhusiano mwema na Vyama vyote vya Siasa vya Nchi nyingine vyenye itikadi kama ya CCM ambavyo kweli vinapinga Ukoloni, Ukoloni Mamboleo, Ubeberu na Ubaguzi wa aina yoyote.