photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo

Home > CHEKECHA

CHEKECHA

MWINGILU NCHEMBA; TUPE KAULI YAKO BAADA YA MAHAKAMA KUMFUTIA RWAKATALE KESI YA UGAIDI

May 18, 2013 Category : 1

Heshima kwenu wanajamvi...
karibia wiki mbili sasa baada ya mahakama kuu kumfutia Lwakatale kesi ya ugaidi. Naamini mwigulu au alikuwa hayuko nchini au ndio kipindi hicho alikuwa anaondoka kwenda China. Tangu maamuzi hayo yatolewe na mahakama hatujasikia kauli ya mwigulu Nchemba iwapo atamshawishi DPP akate rufaa au mikanda aliyonayo inao ushahidi zaidi wa kuishawishi mahakama ione hatia ya ugaidi kwa Lwakale. 
Hebu ajongee hapa atoe kauli yake...

HII NDIYO KAULI YA MHESHIMIWA ZITTO KABWA KUTOKANA NA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE

Feb 19, 2013 Category : 0

Matokeo yaKidato cha Nne ya namna hii (zaidi ya nusu ya wahitimu kupata sifuri) na takribani asilimia 90 kufeli kwa kupata daraja la nne na daraja la sifuri ni mwaka tatu sasa mfululizo. Matokeo yakitoka tunasema weeee mpaka povu linatoka. Baada ya wiki tumeshasahau na hakuna hatua yeyote. Lazima Uwajibikaji utokee.

kwanza Waziri lazima awajibike na Naibu wake na Katibu Mkuu na Kamishna. Najua kuwa haina uhusiano wa moja kwa moja maana matatizo ya elimu ni makubwa sana nchini. Lakini ni lazima kitu fulani kitokee ili kufanya mabadiliko. Uwajibikaji ni njia mojawapo inayoleta nidhamu na 'urgency' katika utendaji kazi.

Tumwambie Rais aichukue Wizara ya Elimu, yaani Waziri wa Elimu awe yeye (kuwe na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Elimu). Tumwambie matokeo yakibaki hivi mwakani na yeye atatoka. Najua wa mwakani ndio wapo kidato cha nne sasa na wana msingi mbaya tayari lakini sio jukumu letu kujipa majibu bali ni jukumu letu kuiambia Serikali hapana. Tuwape Masharti. Vinginevyo haya yatakwisha na mwakani itakuja nk.

Hawa watoto wanakwenda wapi? Mwaka jana tulisema mpango wa kujenga vyuo vya ufundi kila Halmashauri ya Wilaya uanze mara moja. Katika Bajeti Kivuli mwaka 2011 tulipiga hesabu kwamba tunahitaji tshs 720 bilioni katika kipindi cha miaka 5 ijayo kujenga vyuo vya ufundi vya VETA kila Wilaya. Tukawaambia badala ya kukopa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kulipana posho ni vema tukope kuwekeza kwenye elimu maana Elimu ni Hifadhi ya Jamii. Elimu yetu ya sasa inazalisha matabaka kwneye jamii na ni hatari sana kwa uhai wa Taifa.

Tunaweza kujidai kujenga madaraja na miji mipya. Tunaweza kujidai kujenga mabomba ya gesi na kusambaza umeme kila kijiji mpaka kwenye vyoo. Kama hakuna Elimu haya yote ni bure kabisa. Hata kukosa uvumilivu wa kiimani sasa hali itakuwa mbaya zaidi unapokuwa na Taifa la mambumbumbu. Waziri Kawambwa na wenzake watoke. Watoke SASA

DR DALALY KAFUMU SIUTAKI UBUNGE.. NALAZIMISHWA

Jan 10, 2013 Category : 0


Aliyekuwa Mbunge wa Igunga,Dr.Dalaly Peter Kafumu, amedai kuwa kwasasa yeye hataki Ubunge lakini CCM inamlazimisha kukata na kuishughulikia rufaa yake dhidi ya kuvuliwa Ubunge huo na Mahakama Kuu. Nikizungumza naye hivi punde, Dr.Kafumu ameilalamikia CCM kwa kuwakosesha Mbunge wana-Igunga kwa kung'ang'ania rufaa ya Ubunge isiyo na tija.

'Sikia Ndugu yangu,mimi kwasasa nimejielekeza kwenye 'profession' yangu.Sitaki hata kusikia Ubunge wala nini sijui. Washauri Viongozi wetu wakubali Jimbo litangazwe wazi na uchaguzi ufanyike upya ili wana-Igunga wawe na Mbunge. Nilishakubali matokeo ya Mahakama.' alisema Dr.Kafumu

'Niliandika kuwafahamisha viongozi wangu. Sasa kwanini hawataki kunielewa? Kwanini wananilazimisha? Kwanini wanang'ang'ania jambo hili? Hawa watu sijui wakoje?!' alisikika Dr.Kafumu kwa sauti ya kukwazika.

Jambo gani liko nyuma ya Jimbo hili la Igunga?

MABOMU YATUMIKA KWA RAIA SOKO LA NGUZO NANE SHINYANGA

Jan 8, 2013 Category : 0


Naombeni nianze kuuliza swali hili..

"Hivi serikali yetu haina njia za kidiplomasia kutatua ama kupata suluhu ya migogoro inayokuwa inajitokeza kati ya wananchi na serikali?"

Nilichokishuhudia leo takribani kwa masaa mawili, katika soko la Nguzo nane mjini Shinyanga ni dhahiri kuwa serikali yetu ni ya kibabe. Hivi na wafanyabiashara wadogowadogo wamekuwa wa kufukuzwa kwa mabomu? Hivi haya mabomu hayana gharama hata yatumike kiholela namna hii!

Nasikitika sana, kitendo cha serikali kuwafanya wananchi kuwa kama wanyama.

Tafakarii..

ENEO LA BANDARI YA MALINDI ALILOKABIDHIWA BAHRESA

Jan 7, 2013 Category : 0


Said Bakhresa na Rais wa Zanzibar Dr Shein

Kitambo kulikuwa na taarifa za kuendeleza eneo la bandari ya malindi hasa lile eneo la boti ndogo ziendazo kwa kasi. Kutokana na Serikali kutokuwa na uwezo hali iliyopelekea kushindwa kuliendeleza iliamua kumkabidhi mfanya biashara mzalendo, Bw Said Bakhresa.
Kutokana na uwezo na uzowefu wake pia mchango wake mkubwa aliofanya katika ukombozi wa usafiri baharini, Bw Bakhresa ameweza kuliendeleza eneo la bandari kule Daressalam kwa kuweka system nzuri na za kisasa. Hivyo kuonyesha moyo wa kutaka kuliendeleza eneo la bandari ya Zanzibar, vilevile.
Hapo mwanzo alikabidhiwa eneo la kuegesha meli, baadae akaruhusiwa kufanya ujenzi wa eneo la kupumzikia wageni, hapohapo bandarini.
Hivi Sasa Bw Bakhresa amekabidhiwa eneo lote la bandari kuanzia kwenye Chuo cha Sayance Baharini hadi kwenye round about ya kuingilia Bandari kuu. Juzi tu alikuwa na ziara ya kupitia na kutembelea eneo hilo na kujionea ujenzi unavyoendelea.
Sio wazo baya hasa Bw Bakhresa akiwa mzawa mwenye uchungu na nchi yake, swali langu ni kuwa jee utaratibu wa kukabidhiwa eneo hili umefuatwa?
Hivi kwanini kila kitu kifanyika kimya kimya hali ya kuwa tunaimarisha utawala bora chini ya misingi ya accountability and transparency?
Jee tungelitangazia eneo hili hivi asingetokezea mwekezaji mwengine hata asiwe mzawa lakini uwekezaji wake ukawa na faida kubwa na nzuri zaidi kuliko huu wa mzawa?


Naomba majibu yenu

KWANINI ATCL WAHUDUMU WA NDEGE NI WAZUNGU, WACHINA NA WAKOREA??.. CHEKI PICHA HIZO.

Jan 5, 2013 Category : 0


Nimebahatisha juzi kwa mara ya kwanza kupanda ndege za ATCL mhhhh maajabu nliyoyaona;
1. wahudumu ni wachina, korea na wazungu
2. wahudumu wa kiume wana Vitambi hii sio ishu
3. Huduma unapewa moja mfano chakula aina moja huna option, no wine no nini hahah
4. Hakuna hata vijarida vya kusoma wakati wa uchovu au hata manual zinazoonesha vivutio vya ndani mh hhh
Wadau ni mapungufu nimeyaona japo ntazidi kupanda ATCL kuwaunga mkono.
Swali je WATANZANIA hamkuomba kazi au ndo ......